Tuesday, December 1, 2015
vijue vyakula vya kukuza nywele
KILA MTU ANA UWEZO WA KUWA NA NYWELE NZUZI NA ZENYE AFYA CHA MSINGI NI KUJUA MASHART YA KUZIFANYA ZIKUE NA ZISIKATIKE
vitamins ni vitu muhimu sana kwenye ukuaji wa nywele na kama una ukosefu wa VITAMIN huwezi kuwa na nywele ndefu na zenye afya. Vitamin muhinu kwa nywele ni A,C,D K na B zote kuanzia B1-B12
VITANIN A
vitamin A inasaidia kuchochea upatikanaji wa mafuta ya asili ya kwenye ngozi ya kichwa hivyo kuondoa ukavu wa ngozi ya kichwa na kusaidia nywele kurefuka haraka na kutokatika. unaweza kupata vitsmin A kwenye vysakula vifuatavyo;
-maini(mafuta)
-karot
-spinach
-matunda yenye rangi ya peach(rangi kama ya karot)
*unaweza pia kutumia vidonge*
VITAMIN B COMPLEX
Vitamin B inasaidia nywele kuwa ngumu na inayovutika bila kukatika.
- dengu
-kiini cha yai
-glucose
-maini
- njegere
-ngano
-kwenye hamira
*unaweza pia kutumia vidonge*
KUMBUKA;
-kunywa maji mengi kwa sababu yanasaidia damu na virutubisho vilivyomo mwilini kusafiri haraka na kwa ufasaha. pia husaidia ngozi kuwa na unyevu muda wote hivyo nywele hazitakauka sana na wala hazitakatika
-usipende kukausha nywele kwa vifaa vya moto. Unaweza kuosha nywele zako ukakausha kwa taulo then zisuke mabutu mpaka kesho yake zimekauka vizuri.
-Usiweke dawa mara kwa mara zitafanya nywele ziwe nyepesi sana mwisho zinakatika. kam nywele zako zinaota haraka sana na huwezi kuchana, jaribu kutumia chanuo kubwa kuchana nywele za ndani kwa kuzipanga mafungu na zikishalainika pitisha kitana cha kawaida.
- kuwa makini na nywele zenye rangi. kama nywele zina rangi ni rahisi sana kukatika unapoweka dawa. kama umeweka rangi jariku kukaa muda kidogo(miezi 3) ndio uweke dawa.
Jaribu kuvaa kofia au kufunga kitambaa cha silk wakati wa kulala kwa sababu silik inahifadhi unyevu wa asili wa nywele hivyo kuzuia kukatika. Kama huwezi jaribu kulalia mto wa silk badala ya cotton mana cotton inanyonya unyevu na mafuta ya nywele mwisho zinakuwa kavu na kukatika
-Usioshe nywele na sabuni ya kawaida, tumia shampoo na pia uzifanyie conditional mwenyewe na steaming na sio lazima uende saloon. unaweza kununua vifaa vyako ukawa unafanya mwenyewe kila ukiosha( KAMA UNAWEKA CONDITIONAL KILA UNAPOENDA SALOON TU USITEGEMEE KUWA NA NYWELE NZURI. JARIBU KUWEKA KILA UNAPOOSHA MWENYEWE UTAONA MATOKEO)
*SIKUFAFANUA VITAMIN ZOTE NILIZOTAJA HAPO JUU MAA WENGI TUNAZIFAHAMU NA JINSI YA KUZIPATA
Labels:
NYWELE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment