ANGALIA HATUA MOJA BAADA YA NYINGINE
hapa ndio zinavyoonekana kabla sijaanza shughuli
hivi ndio vitu nitakavyochanganya ili kutengeneza conditional, shea butter moistulizer inasaidia kuondoa ukavu kwenye nywele, extra virgin olive oil inalainisha ngozi ya kichwa na inafanya nywele zilainike,conditional yenye alovera inasaidia kujaza nywele na kulainisha pia kufanya nywele zing'are, almond oil inakuza nywele haraka sana,asali inasaidia kuongeza unyevu kwenye nywele, yai na parachichi zina protin nzuri kwa nywele na ngozi
hapa ndio matokeo ya mchanganyiko wangu, nilitumia brenda kusaga na nikahakikisha vimelainika vizuri na hakuna nyuzi nyuzi za parachichi, kila kitu nimeweka kiasi kidigo tu kulingana na uwing au urefu wa nywele zangu ili kuhakikisha kiasi ninachopima kitatosheleza kwa nywele zote
hapa nipo tayari kwa kuosha nywele zangu
hizi ndio shampoo zangu ninazotumia,nazi inalainisha nywele na inakuza nywele,alovera inalainisha,inajaza nywele na kuzifanya zing'are. Unaweza kutumia shampoo yoyote unayotaka. sio kwamba natumia zote kwa wakati mmoja bali natumia moja tu nitakayopenda siku ya kuosha
baada ya kuosha napaka conditional niliyotengeneza kwa mafungu na kila fungu naalinyonga ili kuzuia kushikana wakati wa kuosha pia inasaidia kunyoosha nywele
baada ya kupaka conditional nagfunga kwa mfuko wa plastic ili kuzifanya zipate joto na ifanye kazi haraka
baada ya kufunga na mfuko naweka kitambaa juu kuongeza joto zaidi. Kama utapata kitambaa cha silk ni vizuri zaid maana kinasaidia kuogeza joto na kuzuia kunyonya unyevu halisi wa kwenye nywele. Kaa kwa muda wa nusu saa au zaidi kisha osha.
hizi hapa ndio napaka ndio napaka baada ya kuosha conditional halafu nanyonga tena nywele zangu ili kesho yake zisiwe zimejifunga. Hizi products ni nzuri sana kama ukizipata zitakusaidia sana. Huwa sikaushi nywele kwa moto wa aina yoyote, nikishapaka hizi products nafunga kitambaa changu cha silk nalala. Asubuhi zikiwa zimeshakauka naweka mafuta ya maji. UNAWEZA KUWEKA YOYOTE UNAYOPENDA WEWE.
No comments:
Post a Comment