Monday, February 22, 2016

JINSI YA KUONDOA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA

SABABU NA JINSI YA KUONDOA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA


SABABU
wengi wanadhani sababu ya weusi kati kati ya mapaja ni uchafu lakini sio kweli bali weusi unasababishwa na
-msuguano wakati wa kutembea
-pedi wakati wa hethi (wengine zinawachubua hasa ukivaa muda mrefu na pakipona panakuwa peusi)
-unene
-kutokuwa na uwiano wa hormone za kike (progesterone and estrogen)



JINSI YA KUONDOA WEUSI
*kawaida kwa watu wanene ni ngumu kidodo ila kwa wembamba ni rahisi sana*

*vifaa
SIKU YS KWANZA
-juice ya limao
-mafuta ya nazi
-vaseline au lotion(itazuia msuguano)
       * jinsi ya kutumia
             -mafuta ya nazi kijiko cha chakula 3
             -juice ya nusu limao
              **changanya kisha paka sehemu husika kwa muda wa dakika 15 kisha osha kausha ngozi yako   kisha upake vaseline au lotion

SIKU YA PILI
-sukari
-asali
-limao
        *jinsi ya kutumia
              -sukari kijiko cha chakula 1
              -asali kijiko cha chakula 1
              **changanya kisha paka sehemu husika kwa muda wa dakika 10 kisha osha kausha ngozi yako   kisha upake vaseline au lotion

SIKU YA TATU
 -limao kama kawaida nusu

 -kiazi
        *jinsi ya kutumia
           -kata kiazi katikati halafu sugua sehemu husika kama vile unapaka kwa muda wa dakika kama moja
            **osha na upake juice ya limao ikae kwa muda wa dakika 10 au zaidi then osha kausha ngozi yako na upake vaseline au lotion

[hii ya siku ya tatu utaendelea nayo mpaka uone matokeo]


'ONYO'
--usije ukajaribu kutumia cream ya kuchubua kuondoa weusi maana pakija kusuguana patakuwa pekundu, patachubuka, utapata vidonda, maumivu na unaweza kusababisha matatizo makubwa






1 comment: