Thursday, October 1, 2015
HABARI
HABARI KUTOKA MAGAZETINI LEO TAR 1/10/2015
Kwa habari za chini chini zilizosikika ni kwamba sherehe ya mtoto wa diamond ya kutimiza siku 40 imeacha deni la zaidi ya 1,005,000 za kitanzania. Inasemekana kwamba mpambaji wa shughuli hiyo ambaye pia ni mtangazaji wa tv na redio ambaye jina lake linaanzia na herufi R hakulipwa pesa zake. Mpambaji huyo amedai kwamba tangia shughuli hiyo ifanyike inakaribia wiki mbili sasa na hakuna dalili za kulipwa. Kwa habari zaidi soma gazeti la AMANI.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ASEMA MASOKO YA PEMBE ZA NDOVU NA FARU YAFUNGWE
Akiwa New York rais Kikwete aliwataka wabunge wa bunge la Marekani kufunga masoko ya pembe za ndovu na faru duniani kote ili kuzuiya ujangili uliokithiri katika nchi za Africa. Rais Kikwete ameomba pia msaada wa kifedha utakaoziwezesha nchi za Africa kupambana na ujangili huo. Habari kamili ipo kwenye gazeti la MTANZANIA
NEC; WALIOPOTEZA VITAMBULISHO WATAPIGA KURA
Tume ya uchaguzi NEC wamesema waliopoteza vitambulisho wataruhusiwa kupiga kura endapo watakuwa na taarifa kutoka polisi na majina yao yakiwemo kwenye daftari la mpiga kura. Soma zaidi kwenye gazeti la MTANZANIA
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment